Eutimi abati

(Elekezwa kutoka Eutimi Mkuu)

Eutimi abati (pia: Eutimi mkuu; Melitene, Armenia, leo nchini Uturuki, 377[1][2] - 20 Januari 473) alikuwa mmonaki tangu utotoni, halafu padri na hatimaye abati nchini Palestina, alipokwenda kwa siri akiwa na umri wa miaka 30.

Picha takatifu ya Mt. Eutimi.

Hadi kifo chake alikuwa na unyenyekevu na upendo mkubwa, pamoja na kufuata nidhamu. Kutokana na umaarufu wake, alihamahama sehemu mbalimbali za nchi hiyo ili kukwepa umati uliomtafuta upwekeni[3][4][5][6].

Alipinga uzushi wa Eutike uliolaaniwa na mtaguso wa Kalsedonia (451) akafanya wamonaki wengi na hata malkia wamfuate katika imani sahihi.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Januari [7].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.