Eutropi wa Orange

Eutropi wa Orange (alifariki Orange, Provence, leo nchini Ufaransa, 475 hivi) alikuwa kabaila wa Marseille, huko Ufaransa.

Picha takatifu ya Mt. Eutropi katika kanisa kuu la Orange.

Baada ya kufiwa mke wake, aliyekuwa amemvuta katika Ukristo kutoka maisha ya anasa, akawa shemasi[1] na hatimaye askofu wa Orange tangu mwaka 463 hadi kifo chake[2][3].

Mwandamizi wake, Vero wa Orange, aliandika habari za maisha yake[4].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni 27 Mei[5].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.