Fortunato wa Fano

Fortunato wa Fano (aliishi karne ya 6) alikuwa askofu wa Fano katika Italia ya Kati[1].

Alijitahidi kukomboa watumwa hata kwa kuingia madeni ambayo Papa Gregori I alimruhusu kuyalipa hata kwa kuuza vyombo vya ibada.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 8 Juni[2].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.