Gaugeriki wa Cambrai

Gaugeriki wa Cambrai (pia: Gery, Gorik, Gau; Carignan, leo nchini Ufaransa, 550 hivi - Cambrai, Ufaransa, 11 Agosti 619) alikuwa askofu wa mji huo kwa miaka 39 hivi[1][2].

Mchoro mdogo wa Mt. Gaugeriki.

Maarufu kwa moyo wa ibada na upendo kwa fukara, kwanza alipewa na Magneriki wa Trier ushemasi, halafu akachaguliwa kuwa askofu.

Alianzisha monasteri na kukomboa watumwa pamoja na kuinjilisha hata vijijini[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Agosti[4].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.