Gladys Ngetich

Mhandisi wa Kenya aliyebobea katika uhandisi wa anga

Gladys Chepkirui Ngetich, (alizaliwa mwaka 1991) ni mhandisi wa nchini Kenya, na mwanazuoni wa Rhodes, [1] [2] anaesoma shahada ya udaktari katika uhandisi wa anga katika Chuo Kikuu cha Oxford, nchini Uingereza. [3] [4] Yeye ndiye mpokeaji wa Ushirika wa Tanenbaum na Tuzo la Ubora la Babaroa. [5] [6]

Gladys Chepkirui Ngetich

Historia na elimu

Ngetich alizaliwa katika Kijiji cha Amalo, Kaunti ya Nakuru . Alisomea Shule ya Msingi ya Lelaibei huko Olenguruone. Alisoma katika Shule ya sekondari ya Wasichana ya Mercy huko Kericho . [7] Alidahiliwa katika Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta, na kuhitimu shahada ya Sayansi katika uhandisi wa mitambo, mwaka 2013.

Maisha binafsi

Kama ilivyoelezwa katika Nature, Ngetich anafurahia kukimbia, muziki wa dansi wa Bongo na hip-hop ya Kiswahili. [8]

Viungo vya nje

Marejeo

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gladys Ngetich kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.