Gonzalo Garcia
(Elekezwa kutoka Gonsalo Garcia)
Gonzalo Garcia (1556 - 1597) alikuwa bradha wa shirika la Ndugu Wadogo Pekupeku kutoka India na mmisionari aliyefia dini Japani .
Dhuluma dhidi ya Wakatoliki zilipozidi, yeye na wenzake 25 (mapadri na watawa 8 na walei 17[1]) walikamatwa, walitukanwa na kuteswa vikali, na hatimaye wakasulubiwa huko Nagasaki tarehe 5 Februari mwaka 1597, huku wakifurahia neema ya kuuawa namna ileile ya Yesu.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini. Ni wa kwanza kutangazwa kati ya wazaliwa wa India.
Sikukuu yake na ya wafiadini wenzake huadhimishwa kila mwaka tarehe 6 Februari[2].
Tazama pia
Tanbihi
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoFasihi simuliziAina za manenoShairiVivumishiMikoa ya TanzaniaOrodha ya makabila ya TanzaniaOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaLughaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoKamusi za KiswahiliMofimuFasihiNembo ya TanzaniaMawasilianoSentensiMarie AntoinetteKamusiMange KimambiKumaViwakilishiAlama ya uakifishajiKitenziFani (fasihi)TamthiliaVitendawiliNominoKiswahiliMaudhuiSilabiTanzaniaJumuiya ya Afrika MasharikiKisaweVieleziYoung Africans S.C.Kiwakilishi nafsiDiamond Platnumz