Hesiki wa Gaza

Hesiki wa Gaza (alifariki Maiuma, Palestina, karne ya 4) alikuwa mkaapweke mwanafunzi wa Hilarioni wa Gaza, aliyefuatana naye katika safari zake kwenda Misri, Sicilia, Dalmatia na Kupro.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Oktoba[1][2].

Vyanzo

Chanzo kikuu cha maisha yake ni kitabu cha Jeromu kuhusu Hilarioni [3] kilichoandikwa mwaka 390 huko Bethlehemu kwa lengo la kuhimiza umonaki.[4]

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.