Isaka wa Ninawi

Isaka wa Ninawi (kwa Kiaramu ܡܪܝ ܐܝܣܚܩ ܕܢܝܢܘ; kwa Kiarabu: إسحاق النينوي Ishak an-Naynuwī; kwa Kigiriki Ἰσαὰκ Σύρος, Isaac Syuros; kwa Kiingereza Isaac of Nineveh[1][2][3]; 613 hivi – 700 hivi) alikuwa mwanateolojia na askofu wa Kanisa la Asiria.

Ni maarufu hasa kwa maandishi yake juu ya maisha ya Kiroho. Yapo hadi leo katika lugha asili ya Kisiria na katika tafsiri za kale za Kigiriki na Kiarabu. Yametumiwa sana na Wakristo wa madhehebu mengine, hasa ya Mashariki.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, katika Kanisa lake na makanisa ya Waorthodoksi wa Mashariki na Waorthodoksi.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Januari.

Maisha

Alizaliwa Beth Qatraye, kati ya Mesopotamia na Arabia (Qatar ?)[4][5][6].

Akiwa bado kijana sana alijiunga na monasteri akafanya bidii sana. Akitumia pia maktaba iliyokuwepo, alijipatia sifa upande wa teolojia akaanza kufundisha dini katika eneo lake asili.

Patriarki Georges alipotembelea eneo hilo katikati ya karne ya 7 ili kushiriki sinodi, alimfanya Isaka kuwa askofu wa Ninawi, Assyria, mbali sana, katika Mesopotamia ya Kaskazini.[7].

Majukumu hayo mapya hayakufaa tabia yake, hivyo baada ya miezi 5 alijiuzulu akarudi kusini katika upweke wa Mlima Matout. Huko aliishi miaka mingi akila mikate 3 tu kwa juma pamoja na mboga kidogo.

Hatimaye uzee na upofu vilimlazimisha kurudi monasterini. Huko Shabar alifariki na kuzikwa.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.