Joji wa Antiokia

Joji wa Antiokia (alifariki uhamishoni, karne ya 9) alikuwa mmonaki, halafu askofu wa Antiokia wa Pisidia[1].

Alidhulumiwa na makaisari Konstantino V[2] na Leo V wa Bizanti[3] kwa sababu ya kuheshimu picha takatifu kama ilivyopitishwa na Mtaguso wa pili wa Nisea (787), ambao yeye aliushiriki[3] [4].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Aprili[5].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  • Watkins, Basil (2015). The Book of Saints: A Comprehensive Biographical Dictionary. Bloomsbury Publishing. 
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.