Karpo, Papilo na wenzao

Karpo, Papilo na wenzao (walifariki Pergamo, katika Uturuki ya leo, 170 hivi au 250 hivi) walikuwa Wakristo waliouawa kwa ajili ya imani yao katika dhuluma ya kaisari Marko Aurelio au Decius[1].

Karpo alikuwa askofu wa Gurdos, Lidia, Papilo alikuwa shemasi wa Tuatira na Agatonika dada yake. Wafiadini wenzao wengi hawajulikani kwa jina[2].

Masimulizi ya kifodini chao yametufikia.

Tangu kale wote wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 13 Aprili[3].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.