Kwadrato wa Utica

Kwadrato wa Utica (alifariki 21 Agosti 258 au 259) alikuwa askofu wa mji huo (leo nchini Tunisia) aliyeuawa huko, wakati wa dhuluma ya kaisari Valerian, siku nne baada ya waumini wake wote (Massa Candida).

Augustino wa Hippo alitoa hotuba kwa sifa yake.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Agosti[1][2].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.