Leonidas wa Aleksandria

Leonidas wa Aleksandria (kwa Kigiriki: Λεωνίδης, Leonides; alifariki 202) alikuwa Mkristo wa Misri ambaye alifia dini yake kwa upanga wakati wa dhuluma ya kaisari Septimius Severus[1].

Origen, mtoto wa Leonidas.

Leonidas alimsaidia mwanae Origen kujiendeleza kadiri ya akili yake kubwa ajabu na kujua Biblia tangu utotoni[2]. Baada ya huyo, alizaa walau watoto wengine sita[3][4].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu[5].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Aprili[6][7].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.