Listra

Listra (kwa Kigiriki: Λύστρα, Lyustra) ulikuwa mji wa rasi ya Anatolia, katika Uturuki wa leo.

Mt. Paulo na Mt. Barnaba kuko Listra, mchoro wa Willem de Poorter, 1636.

Kwa sasa ni kijiji tu kinachoitwa Klistra, km 30 kusini kwa Konya[1].

Mji huo unatajwa mara sita katika Biblia ya Kikristo (Mdo 14:6,8,21; 16:1, 2Tim 3:11) kwa sababu kuanzia mwaka 46 Mtume Paulo alifika huko mara kadhaa kuinjilisha akiwa mara na Barnaba, mara na Sila[2]. Ndipo alipomkuta Timotheo ambaye akawa mshirika na hatimaye mwandamizi wake.

Tanbihi

Viungo vyanje

Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Listra kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.