Lonjino wa Pamaria

Lonjino wa Pamaria (alifariki 483) alikuwa askofu wa Pamaria (leo nchini Algeria) hadi alipopelekwa uhamishoni katika kisiwa cha Corsica (leo nchini Ufaransa) kutokana na dhuluma za Wavandali Waario dhidi ya Wakatoliki. Ilikuwa vilevile kwa maaskofu wengine 650.

Baada ya kuinjilisha kisiwa hicho pamoja na maaskofu Vendemiale, Eujeni wa Karthago, hatimaye alifia dini kwa kukatwa kichwa kwa amri ya mfalme Huneriki.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Mei[1][2].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.