Mariano wa Bourges

Mariano wa Bourges (aliishi Bourges, Ufaransa, karne ya 6) alikuwa mkaapweke aliyeshika maisha magumu sana kwa miaka 44, akila tu matunda ya porini na asali aliyoiona bila kufuga nyuki.

Mt. Mariano katika kioo cha rangi cha kanisa la Mézilles.

Kabla ya hapo aliwahi kuoa, halafu kuishi monasterini miaka sita[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Septemba[2][3].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  • Jean Dequaire, Saint Marien, ermite d’Entraigues, protecteur d’Évaux.
  • Georges Piquand, Légendes bourbonnaises, réimpr. Marseille, Laffitte, 1978 : « Légendes de saint Marien et du diable ».
  • Maurice Piboule, « St Marien et Ste Radegonde en Bourbonnais », Bulletin de la Société de mythologie française, 1979, vol. 113, Kigezo:P..

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.