Maruta

Maruta (karne ya 4415) alikuwa mmonaki wa Kanisa la Mashariki[1] maarufu kama askofu wa Mayferkat (leo Silvan nchini Uturuki) kwa zaidi ya miaka 10 ambapo alifaulu kuzuia dhuluma ya Dola la Persia dhidi ya Wakristo[2].

Mchoro mdogo ukimwonyesha Mt. Maruta askofu.

Hivyo aliweza kujenga upya makanisa, kukusanya humo masalia ya wafiadini, kuendesha sinodi mbili zilizolipa Kanisa hilo muundo imara, pamoja na kuandika vitabu vya historia ya Kanisa na ufafanuzi wa Biblia, tenzi, anafora n.k.[3]

Rafiki wa Yohane Krisostomo, alishiriki Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (481)[4].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Februari[5].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  • Maruthas from the Catholic Encyclopedia (1915)
  • De Lacy O'Leary, The Syriac Church and Fathers (2002)
  • Smith, William & Wace, Henry (editors); A dictionary of christian biography, literature, sects and doctrine, "Maruthas (1)", (1877).
  • Moffett, Samuel Hugh. A History of Christianity in Asia, (Maryknoll: Orbis Books, 1998) p. 154-155
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.