Maryahb

Maryahb (jina lake linamaanisha “Mungu anapanga”; alifariki nchini Uajemi, 341) ni kati ya Wakristo elfu kadhaa, waliouawa kwa sababu ya imani yao katika dhuluma ya mfalme Sabor II [1].

Maryahb alikuwa padri korepiskopo na aliuawa katika Oktava ya Pasaka[2].

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Aprili[3].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.