Nikola wa Flue

Nikola wa Flue (kwa Kijerumani: Niklaus von Flüe; Unterwalden, Uswisi, 1417 - Sachseln, 21 Machi, 1487) alikuwa Mkristo anaheshimiwa na Wakatoliki na Waprotestanti kama msimamizi wa Uswisi kwa kuepusha vita kati ya majimbo yake[1] na hivyo kudumisha umoja wake[2].

Mt. Nikola wa Flue.

Alitangazwa mwenye heri mwaka 1669, halafu mtakatifu mwaka 1947 na Papa Pius XII[3].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[4].

Maisha

Baba wa familia ya watoto kumi, mkulima, mwanasiasa, kapteni, hakimu, mwaka 1467 alifuata wito bora zaidi [5] wa kuishi kama mkaapweke mlimani ingawa huko pia alitafutwa na wengi kutoka nchi mbalimbali kwa ushauri wake[1].

Akidharau kabisa malimwengu, aliacha chumba chake mara moja tu ili kupatanisha watu na hivyo kuepusha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini.

Maarufu kwa ukali wa toba yake, ulitolewa ushahidi kwa kiapo kwamba kwa miaka 19 hakula chochote ila sakramenti ya ekaristi tu.

Sala yake

Bwana, uniondolee yale yote yanayonizuia nisifike kwako;

unijalie yale yote yanayoweza kunifikisha kwako;

ujichukulie nafsi yangu, na kujipatia kabisa mwenyewe[6].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  • Abel, Winfried, “The Prayer Book of St. Nicholas of Flue: Mystery of the Center”, Christiana Edition, Stein Am Rhein, 1999.
  • Boos, Thomas, “Nicholas of Flue, 1417-1487, Swiss Hermit and Peacemaker”, The Pentland Press, Ltd, Edinburgh, 1999.
  • Collins, David J. "Turning Swiss: The Patriotism of the Holy Hermit Nicholas". In Reforming Saints. Oxford: Oxford University Press. 2008. ku. 99–122. 
  • Jung, Carl Gustav, "Brother Klaus", ;;The Collected Works of C. G. Jung;;, Bollingen Series XX, Volume 11, Princeton, 1977.
  • Kaiser, Lother Emanuel, “Nicholas of Flue-Brother Nicholas: Saint of Peace Throughout the World.” Editions du Signe, Strausbourg, 2002.
  • Yates, Christina, “Brother Klaus: A Man of Two Worlds” The Ebor Press, York, England, 1989.
  • “Brother Klaus: Our Companion Through Life”, Bruder-Kalusen-Stiftung-Sachseln, 2005.
  • "The Transformed Berserker: The Union of Psychic Opposites" The Archetypal Dimensions of the Psyche. von Franz, Marie-Louise. Shambhala, 1997.

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.