Niseta wa Remesiana

Niseta wa Remesiana (333 hivi - 414 hivi) kwa miaka hamsini hivi alikuwa askofu wa mji huo (leo nchini Serbia).

Alikuwa mmisionari sehemu za Balkani[1][2][3].

Paulino wa Nola alimsifu katika shairi lake mojawapo kwa kufundisha Injili kwa Wapagani na kuwafanya kondoo wapole wa zizi lenye amani; hivyo waliokuwa kwanza washenzi walioishi kwa wizi, wamejifunza kumuimbia Kristo kwa moyo wa Kirumi[4].

Pia ni maarufu kwa maandishi yake[5] na kwa tenzi za Kilatini alizotunga kwa ajili ya liturujia. Kati yake maarufu zaidi ni Te Deum.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Juni[6].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.