Optatus wa Milevi

Optatus wa Milevi alikuwa askofu wa Milevi, huko Numidia, katika karne ya 4; anakumbukwa hasa kwa maandishi yake bora dhidi ya Parmenianus na wafuasi wengine wa Donato Mkuu[1], ambayo yalisisitiza kwamba Kanisa ni la kimataifa, na kwamba Wakristo wanahitaji sana kuwa na umoja kati yao wote.

Mt. Optatus.

Optatus alikuwa ameongokea Ukristo, alivyoandika Augustino wa Hippo[2], labda baada ya kuwa mtaalamu wa kuhubiri Mpagani.

Tangu kale Optatus anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Juni[3][4].

Tazama pia

Tanbihi

Vyanzo

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.