Plutarko, Potamiena na wenzao

Plutarko, Potamiena na wenzao Sereno, Eraklide, Erone, Sereno, Eraide na Marsela (walifariki Aleksandria, Misri, 202 hivi) walikuwa Wakristo wa mji huo wanafunzi wa Origen walioteswa na hatimaye kuuawa kwa namna mbalimbali kwa ajili ya imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Septimius Severus[1][2].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 28 Juni[3].

Pengine wanatajwa kama wenzao pia Ambeni, Basilide, Irenei, Julius, Leonides, Leonides, Marseli, Menomi, Nonika, Theodori, Pastafi, Titiro, Pasimi, Fesiki, Ariosi, Dioskoro, Orioni, Orioni, Oriosi, Pambani, Panofi, Panumeri, Pece, Plutarko, Potamini, Sidisto, Simeri, Sinido, Tilino, Turbani, Kapitulini, Dionisia, Dista na Rais[4].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.