Polisi

Polisi (kutoka neno la Kiingereza police lilikopwa kutoka Kifaransa police[1] ambalo awali lilikuwa la Kilatini politia,[2] na kabla yake tena la Kigiriki πολιτεία, politeia, "uraia, usimamizi, ustaarabu wa mjini".[3] Msingi ni neno πόλις, polis, "mji".[4]) ni idara ya serikali ambayo lengo lake ni kutekeleza sheria za nchi,[5] kulinda mali[6] kudumisha usalama na kupunguza vurugu, kutokomeza vifo visivyokuwa vya lazima, pamoja na kuokoa mali.[7][8]

Askari polisi wa Ujerumani.

Polisi pekee inaruhusiwa kutumia nguvu katika jamii.

Kwa kawaida polisi hutofautiana na wanajeshi ambao kazi yao ni kulinda nchi dhidi ya wavamizi kutoka nje.

Mara nyingi polisi wanajulikana kuathiriwa na ufisadi kwa kiasi tofautitofauti.

Tanbihi