Rabanus Maurus

Rabanus Maurus Magnentius (Mainz, 780 hivi – Oestrich-Winkel, 4 Februari 856), alikuwa mmonaki Mbenedikto maarufu kama mwanateolojia na mhubiri, ambaye akawa askofu mkuu wa Mainz, Ujerumani.

Rabanus Maurus (kushoto) akitoa kitabu chake kwa Otgar wa Mainz.

Ndiye mtunzi wa kamusi elezo De rerum naturis ("Mambo ya uasilia") na wa vitabu mbalimbali kuhusu malezi, sarufi na ufafanuzi wa Biblia[1].

Kwa umuhimu wake kati ya walimu wa kipindi cha Karolo Mkuu, aliitwa "Praeceptor Germaniae" ("mwalimu wa Ujerumani").

Anasifiwa kwa kutoacha chochote alichoweza kufanya kwa utukufu wa Mungu.

Katika Martyrologium Romanum anatajwa kama mtakatifu wa Kanisa Katoliki, sikukuu yake ikiwa tarehe 4 Februari[2].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.