(Beta Pegasi, Scheat) | |
---|---|
Kundinyota | Farasi (Pegasus) |
Mwangaza unaonekana | 2.4 (geugeu 2.3 – 2.7)[1] |
Kundi la spektra | M2 II-III |
Paralaksi (mas) | 16.64 ± 0.15 |
Umbali (miakanuru) | 196 |
Mwangaza halisi | -1.4 |
Masi M☉ | 2.1 |
Nusukipenyo R☉ | 95 |
Jotoridi usoni wa nyota (K) | 3689 |
Majina mbadala | 53 Peg, HR 8775, BD +27°4480, HD 217906, SAO 90981, FK5 870, HIP 113881. |
Saidi (lat. & ing. Scheat pia β Beta Pegasi [2], kifupi Beta Peg’’’, β Peg’’’) ni kati ya nyota angavu za kundinyota ya Farasi (Pegasus).
Jina la Saidi ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [3]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema kwa kawaida الساعد as-sa’id inayomaanisha “mkono" (au mguu wa farasi). Walitafsiri kwa njia hii maelezo ya Ptolemaio asiyetumia jina lakini alieleza “nyota kwenye mbega wa kulia pale ambako mguu unaanza”. [4]
Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu kwa tahajia ya Kijerumani jinsi ilivyokuwa kawaida katika Ulaya na kuorodhesha nyota kwa jina la "Scheat" [5] .
Beta Pegasi ni jina la Bayer ; Beta ni herufi ya pili katika Alfabeti ya Kigiriki na Saidi ni nyota angavu ya pili katika Farasi - Pegasus.
Saidi ni nyota jitu jekundu katika kundi la spektra M2 ikiwa umbali wa karibu miaka nuru 200. Ni pia nyota badilifu ni mwangaza wake unacheza baina ya mag 2.3 na 2.7 kila baada ya siku 41.