Saksonia

Saksonia (pia Saxony. Kijerumani Sachsen, Kisorbia Sakska; jina rasmi Freistaat Sachsen ("Dola Huru la Saksonia") ni moja ya majimbo 16 ya kujitawala ya Ujerumani lenye wakazi 4,173,000 kwenye eneo la 18 415 km². Mji mkuu ni Dresden, mji mkubwa Leipzig. Waziri mkuu ni Michael Kretschmer (CDU). Jimbo liko katika mashariki ya nchi likipakana na Ucheki na Poland. Saksonia ni dola la kale ndani ya Ujerumani, wakati wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani ilifutwa kati ya 1952 hadi 1990 na kugawiwa kwa mikoa mbalimbali.

Uwanja wa timu ya Leipzig ulioko Saksonia
Mahali pa Saksonia katika Ujerumani
bendera ya Saksonia

Jiografia

Saxonia iko mpakani wa Ujerumani na Poland upande wa mashariki na Ucheki upande wa kusini. Majimbo jirani ndani ya Ujerumani ni Brandenburg upande wa kaskazini, Saksonia-Anhalt, Thuringia na Bavaria upanda wa magharibi. Sehemu kubwa ya mpaka wa kusini inapita kwenye safu ya milima ya Erzgebirge.

Maeneo ya kaskazini ni tambarare hasa beseni ya Leipzig. Kusini kuna kanda ya milima inayofikia mita 1215 juu ya UB kwenye Fichtelberg katika Erzgebirge (milima ya madini).

Mto mkubwa ni Elbe unaopita jimbo lote likipitika kwa meli za mtoni.

Miji

MjiWilayaWakazi
31 Desemba 2000
Wakazi
31 Desemba 2006
Wakazi
30 Juni 2008
LeipzigLeipzig (jiji)493,208506,260511,676
DresdenDresden (jiji)477,807504,635508,398
ChemnitzChemnitz (jiji)259,246245,739244,310
ZwickauZwickau (wilaya)103,00896,87895,322
PlauenVogtlandkreis (wilaya)71,54368,31767,309
GörlitzGörlitz (wilaya)61,59957,20156,608
HoyerswerdaBautzen (wilaya)50,20341,51539,835
FreibergMittelsachsen (wilaya)45,42842,77242,120
BautzenBautzen (wilaya)43,35341,76641,354
PirnaSächsische Schweiz-Osterzgebirge (wilaya)42,10839,74839,291
FreitalSächsische Schweiz-Osterzgebirge (wilaya)40,12939,05939,139
RiesaRiesa-Großenhain (wilaya)39,36736,14535,139
RadebeulMeißen (wilaya)32,24633,20533,284
MeißenMeißen (wilaya)29,39828,09127,846
Limbach-OberfrohnaZwickau (wilaya)27,55226,59126,113
ZittauGörlitz (wilaya)27,45424,89229,093
GlauchauZwickau (wilaya)27,28525,74425,159
Delitzsch¹Nordsachsen (wilaya)26,33127,44827,111
Weißwasser/O.L.Görlitz (wilaya)26,10721,79720,298
WerdauZwickau (wilaya)26,07723,97623,565
Annaberg-BuchholzErzgebirgskreis (wilaya)24,49522,81722,514
CoswigMeißen (wilaya)24,03522,36522,514
Reichenbach im VogtlandVogtlandkreis (wilaya)23,46922,16421,210
CrimmitschauZwickau (wilaya)23,30522,33021,684
MarkkleebergLeipzig (wilaya)23,15723,71823,962
DöbelnMittelsachsen (wilaya)23,12821,35620,726
Schwarzenberg/Erzgeb.Erzgebirgskreis (wilaya)20,20118,51719,187
AuerbachVogtlandkreis (wilaya)20,04221,24620,620
BornaLeipzig (wilaya)20,01022,65721,539

Utawala

Saksonia ina mikoa 3 (Chemnitz, Dresden na Leipzig) zenye wilaya 10:

(Alama za magari kwa kila wilaya katika mabano)

  1. Bautzen (BZ)
  2. Erzgebirgskreis (ERZ)
  3. Leipzig (L)
  4. Meißen (MEI)
  5. Mittelsachsen (FG)
  6. Görlitz (GR)
  7. Nordsachsen (TDO)
  8. Sächsische Schweiz-Osterzgebirge (PIR)
  9. Vogtlandkreis (V)
  10. Zwickau (Z)
Districts of Saxony

Majiji

Saksonia ina majiji matatu (katika Ujerumani ila mji mwenye wakazi zaidi ya 100,000 inahesabiwa kma jiji) yenye cheo cha wilaya:

Historia

Leo hii "Saksonia" ni jina la maeneo kwenye pande zote mbili za mto Elbe unapopita kwenye milima ya Erzgebirge mpakani wa Ucheki. Kiasili jina la "Saksonia" ilitaja maeneo ya kaskazini ya Ujerumani walipoishi Wasaksonia ambayo leo hii huitwa "Saksonia ya chini" (Niedersachsen). Cheo cha watemi wa Saksonia kilirithiwa na watawala wa Meißen katika karne ya 15 na tangu wakati ule nchi yao ilianza kuitwa "Sachsen"; kwa uda mrefu Wajerumani walitofautisha kati ya "Saksonia ya Juu" (= Saksonia ya leo) na "Saksonia ya Chini".

Maeneo ya Saksonia ya leo yalikaliwa na makabila ya Kijerumani upande wa magharibi na makabila ya Kislavoni walioitwa "Wasorbi" upande wa mashariki. Polepole Waslavoni wengi walianza kutumia lugha ya Kijerumani lakini hadi leo kuna vijiji kadhaa vyenye wasemaji wengi wa Kisorbi kwa jumla hawazidi watu 20,000.

Saksonia iliweza kutetea cheo chake kama dola la kujitegemea katika historia ya Ujerumani iliyoona harakati ya maeneo madogo kumezwa na madola makubwa zaidi. Wakati wa matengenezo ya kiprotestanti Saksonia ilichagua dhehebu la kilutheri kama dini rasmi.

Mtemi Friedrich August I wa Saksonia ((1670 - 1733) alichaguliwa kuwa pia mfalme wa Poland kwa jina la August II. Alipamba mji mkuu wa Dresden kwa majengo mazuri yaliyounda sifa ya mji kuwa "Firenze kwenye mto Elbe" (Kijerumani: Elbflorenz). Hata mwana wake aliweza kutawala kama mtemi wa Saksonia na mfalme wa Poland lakini baadaye dola likashuka tena cheo kuwa moja ya madola ya Kijerumani ya wastani yaliyojaribu kuhifadhi uhuru wao kati ya madola makubwa Austria na Prussia.

Wakati wa vita za Napoleoni Saksonia ilipambana dhidi ya Mfaransa pamoja na Prussia lakini baada ya kushindwa ikahamia upande wa Naoleoni ikapewa naye cheo cha ufalme. Cheo hiki kilithebitishwa kwenye mkutano wa Vienna mwaka 1815. Hadi 1870 Saksonia ilikuwa ufalme ndani ya Shirikisho la Ujerumani, baadaye ndani ya Dola la Ujerumani.

Mwaka 1918 Saksonia liona mapinduzi sawa na sehemu nyingine za Ujerumani, mfalme wa mwisho akapinduliwa na jamhuri ya "Dola Huru la Saksonia" ikatangzwa kama jimbo ndani ya Jamhuri ya Dola la Ujerumani. Baada ya vita kuu ya pili ya dunia Ujerumani uliawiwa kati ya nchi washindi na Saksonia ilikuwa sehemu ya kanda la Kisovyeti na tangu 1949 sehemu ya Jamhuri ya ya Kidemokrasia ya Kijerumani (Ujerumani ya Mashariki) chini ya utawala wa kikomunisti. 1952 serikali ilifuta muundo wa majimbo Saksonia ikagawiwa kwa mikoa mbalimbali. Wakati wa kuporomoka kwa utawala wa kikomunisti majibo ya awali yaliundwa upya mwaka 1990 na mwaka uleule Saksonia pamoja na majimbo megine ya mashariki ikajiunga na Jamhuri la Shirikisho la Ujerumani katika maungano ya Ujerumani.

Demografia

Mabadiliko ya idadi ya wakazi katika Saksonia tangu 1905:

MwakaWakazi
19054,508,601
19465,558,566
19505,682,802
19645,463,571
19705,419,187
19815,152,857
19904,764,301
19954,566,603
MwakaWakazi
20004,425,581
20014,384,192
20024,349,659
20034,321,437
20044,296,284
20054,273,754
20064,249,774
20074,220,200
20084,192,700

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:



 
Majimbo ya Ujerumani
Baden-WürttembergBavaria (Bayern)BerlinBrandenburgBremenHamburgHesse (Hessen)Mecklenburg-Pomerini Magharibi (Mecklenburg-Vorpommern)Saksonia Chini (Niedersachsen)Rhine Kaskazini-Westfalia (Nordrhein-Westfalen)Rhine-Palatino (Rheinland-Pfalz)Saar (Saarland)Saksonia (Sachsen)Saksonia-Anhalt (Sachsen-Anhalt)Schleswig-HolsteinThuringia (Thüringen)