Saserdosi wa Lyon

Saserdosi wa Lyon (pia: Sardot au Serdot; 487 - 552[1]) alikuwa askofu mkuu wa mji huo, leo nchini Ufaransa [2][3] kuanzia mwaka 544 hadi kifo chake[4][5].

Sanamu ya Mt. Saserdosi katika kanisa la Mt. Paulo, Lyon.

Alikuwa mtoto wa askofu Rustiko wa Lyon ambaye anaheshimiwa kama mtakatifu. Mwenyewe naye, kabla ya kupata uaskofu, aliwahi kuoa na kuzaa mtoto mmoja, Aureliano wa Arles, ambaye pia anaheshimika hivyo [6].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Septemba[7].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.