Timotheo Msomaji

Timotheo Msomaji (alifariki 286) alikuwa Mkristo wa Antinoe, Misri, aliyeuawa kwa ajili ya imani yake pamoja na mke wake Maura wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian[1].

Baada ya kupigiliwa misumari ukutani aliteseka siku 9 kabla hajafa.

Baba yake alikuwa padri Pikolposos. Timotheo alipaswa kunakili na kutunza vitabu vya ibada.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Mei[2].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.