Tipasi

Tipasi (kwa Kilatini: Typasius; alifariki 11 Januari 304) alikuwa askari kutoka Tigava (leo El Kherba, nchini Algeria)[1].

Baada ya kuingia Ukristo na kuacha maisha ya jeshi, alipoitwa na kaisari Maksimiani kusaidia katika vita dhidi ya wenyeji Quinquegentiani waliotaka kupinga mamlaka ya Dola la Roma, Tipasi alikataa[2].

Baadaye alianzisha monasteri alipoishi muda mrefu. Hatimaye aliitwa tena jeshini na kudaiwa kutoa sadaka kwa miungu ya Roma. Hapo akakatwa kichwa.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake, 11 Januari[3][4].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.