Ujana

Ujana ni kipindi cha maisha kati ya utoto na utu uzima.[1][2]

Askari Mnaijeria na marafiki wake.

Unaelezwa kama kipindi cha ustawi wa mwili na wa nafsi tangu mwanzo wa ubalehe kwa ukomavu hadi mwanzoni mwa utu uzima.

Mipaka ya umri

Ufafanuzi wa umri maalumu wa ujana hutofautiana. Ukomavu wa mtu binafsi huenda unakosa kuwa sawa na umri wao, kwani watu wasiokomaa hupatikana kwa umri wowote.

Umri ambao mtu anahesabiwa ni "kijana", na huduma maalumu chini ya sheria na katika jamii unatofautiana duniani kote.

  • "Kijana ... wale watu ambao wako kati ya umri wa miaka 15 na 24." - Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa [3]
  • "Muda katika maisha ya mtu kati ya utoto na utu uzima. Neno "kijana" kwa ujumla linahusu wale walio kati ya miaka 15 hadi 25. "- Benki ya Dunia. [4]
  • Commonwealth Youth Programme kazi na "vijana (umri 15-29)." [5]
  • "Mtu ... chini ya umri wa miaka 21." - National Highway Traffic Safety Administration [6]
  • "Watu kati ya umri wa 14 na 21." - Shule ya Wilson ya Wilaya[7]
  • "Kijana; mtu binafsi kutoka umri wa miaka 13 hadi miaka 19." - Alternative Homes for Youth, Inc [8]

Takwimu

Vijana karibu wote duniani wanaishi katika nchi zinazoendelea: kadiri ya UM, kwa sasa ni 85% wa watu wenye umri kati ya miaka 15 na 24, lakini watafikia 89.5% mwaka 2025.

Uwajibikaji wa vijana

Kila kijana ana wajibu wa kufanya kazi kwa bidii ili maendeleo ya nchi yake yaweze kwenda sawa, kwani kwa kufanya kazi anaepuka zaidi mmomonyoko wa maadili uliokithiri kwa vijana, hasa kuiga mambo ya kigeni yasiyo na manufaa kwao na kwa taifa kwa ujumla.

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ujana kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.