Yohane Gualberto

Yohane Gualberto (995 hivi - 12 Julai 1073) alikuwa mmonaki wa Toscana, Italia ya Kati aliyeanzisha urekebisho wa Vallombrosa.

Mt. Yohane Gualberto. Mchoro wa ukutani wa Neri di Bicci, Santa Trinita huko Firenze.

Kabla ya hapo alikuwa askari kutoka familia maarufu ya Visdomini. Ndugu yake alipouawa, alipaswa kulipa kisasi kwa kumuua muuaji. Alipompata, huyo alimpigia magoti na kunyosha mikono kama Yesu msalabani akimuomba msamaha. Ilikuwa siku ya Ijumaa Kuu. Hapo Yohane alitupa upanga wake na kumkumbatia.

Bernardo Giambullari, Storia e miracoli di San Giovanni Gualberto, ca. 1500

Baada ya hapo alijiunga na monasteri ya Wabenedikto wa San Miniato.

Aliposhindana na abati na askofu wake wenye tabia ya usimoni, ambao yeye aliupiga vita, aliacha jumuia na mwaka 1036 alifika pamoja na wenzake kadhaa huko Vallombrosa [1].

Baada ya Papa kuthibitisha nia yao, shirika lilistawi sana.

Mwaka 1193 alitangazwa na Papa Celestino III kuwa mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Tazama pia

Tanbihi

Vyanzo

  • F. Salvestrini, Disciplina Caritatis, Il monachesimo vallombrosano tra medioevo e prima età moderna, Rome, Viella, 2008.
  • F. Salvestrini, Santa Maria di Vallombrosa. Patrimonio e vita economica di un grande monastero medievale, Florence, Olschki, 1998.
  • Salvestrini, F. (2010). Santa Vallombrosani in Liguria. Storia di una presenza monastica fra Dodicesimo e Diciassettesimo secolo. Rome: Viella. 
  • F. Salvestrini, mhariri (2011). I Vallombrosani in Lombardia (XI-XVIII secolo). Milan-Lecco: ERSAF. 

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.