Tana (ziwa)

(Elekezwa kutoka Ziwa Tana)

Ziwa la Tana ni ziwa kubwa la Ethiopia ambalo ni asili ya Nile ya Buluu. Beseni lake liko takriban km 370 kaskazini-magharibi kwa Addis Ababa katika nyanda za juu za Ethiopia.

Ziwa Tana
Ziwa la Tana, picha kutoka angani, 1991
Ziwa la Tana, picha kutoka angani, 1991
MahaliNyanda za juu za Ethiopia, (Afrika ya Mashariki)
Eneo la maji2.156 km²
Kina cha chini14 m
Mito inayoingiaRib na Gumara
Mito inayotokaAbbai (Nile ya buluu)
Kimo cha uso wa maji
juu ya UB
1.788 m
Miji mikubwa ufukoniBahir Dar

Umbo la ziwa limebadilika katika karne iliyopita kutokana na mashapo. Kamusi ya mwaka 1888 ilitaja kina cha mita 100, lakini leo ni mita 14 pekee. Eneo la ziwa hubadilika na majira ya mvua au ukame yaani kuwa na maji mengi au kidogo.

Mito mingi inaingia ziwani ikiwa mikubwa, kati yake ni mito ya Reb na Gumara.

Mto Abbai (jina la Kiethiopia la Nile ya buluu) unatoka katika ziwa.

Eneo la Ziwa la Tana ni kitovu cha kihistoria cha Ethiopia ya Kikristo. Katika visiwa vidogo ziwani kuna makanisa na monasteri 20 zilizojengwa tangu karne ya 14 BK.

Picha

Viungo vya nje

WikiMedia Commons


Makala hii kuhusu maeneo ya Ethiopia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tana (ziwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.