Nenda kwa yaliyomo

Kona

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kona

Posta ya Kona
Imeongozwa naSalim Ahmed
Imetayarishwa naChristian Komba
Imetungwa naSalim Ahmed
NyotaAhmed Salim
Riyama Ally
Christian Komba
Imesambazwa naSteps Entertainment
Imetolewa tar.30 Mei, 2015
NchiTanzania
LughaKiswahili

'Kona ni jina la filamu iliyotoka mwaka 2015 kutoka nchini Tanzania. Ndani yake anakuja Salim Ahmed (Gabo), Riyama Ally na Christian Komba. Filamu imeongozwa na Gabo na kutayarishwa na Christian Komba huku picha ikipigwa na Landline Production. Filamu ilitengenezwa mwaka 2014 huko wilayani Songea katika mkoa wa Ruvuma na kusambazwa na Steps Entertainment kwa Tanzania nzima. Muswaada andishi umeandikwa na Patrick Komba. Filamu inaelezea umuhimu wa malezi ya pande zote mbili za wazazi ili kusimamia elimu imara kwa mtoto.[1][2]

Hadithihariri chanzo

Kijana Zazuba aliyekuwa anaishi na mjomba wake, hakuwa na kipato kikubwa lakini malengo yake yalikuwa mwanaye asome hadi Chuo Kikuu. Kwa mujibu wa sheria mtoto huyo iliamriwa akae na mama yake. Mtoto huyo anakosa uangalizi mzuri katika masomo yake na umakini katika malezi maana muda mwingi bibi na mama yake wana shughuli nyingi za biashara ya pombe. Siku moja mtoto anakunywa pombe ya gongo iliyoachwa na mlevi, mwishowe anapoteza maisha kwa ungalizi mdogo.

Washirikihariri chanzo

  • Salim Ahmed
  • Riyama Ally
  • Christian Komba

Marejeohariri chanzo

Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kona kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoShairiJumuiya ya Afrika MasharikiUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaFasihi simuliziNembo ya TanzaniaMshororoMikoa ya TanzaniaVivumishiOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoPentekosteAina za manenoTanzaniaKamusi za KiswahiliMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaOrodha ya makabila ya TanzaniaAfrika Mashariki 1800-1845Orodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaUpendo Furaha PenezaMafurikoMisimu (lugha)KumaKisaweSentensiDiamond PlatnumzKamusi ya Kiswahili sanifuKamusiMisemoMaudhuiSimba S.C.Ukwapi na utaoTanganyikaOrodha ya Watakatifu WakristoNgeliLahaja za KiswahiliMaumivu ya kiunoRoho MtakatifuNomino