Nenda kwa yaliyomo

Walombardi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hatua kuu za uhamaji wa Walombardi kutoka Uswidi hadi Italia.
Utawala wa Walombardi Italia (samawati) ilipofikia kilele chake (751).

Walombardi (au Walongobardi, kutoka Kilatini Langobardi, yaani "wenye ndevu ndefu") walikuwa moja kati ya makabila ya Kijerumani[1][2][3][4][5].

Kutoka Uswidi[6][7] walianza kuelekea kusini na kati ya karne ya 2 hadi karne ya 6 walifika hadi Italia ambayo waliiteka kuanzia mwaka 568 na kuitawala kwa kiasi kikubwa hadi waliposhindwa na Karolo Mkuu mwaka 774.

Hata hivyo katika Italia Kusini walidumu kutawala maeneo mapana hadi karne ya 11 walipozidiwa na Wanormani. Jambo hilo lilifanya wakazi wengi wabaki nje ya utawala wa dola la Bizanti na Ukristo wa Mashariki.

Hasa baada ya kuacha Uario na kujiunga na Kanisa Katoliki, Walombardi walichanganyikana na wenyeji. Kwa kuwa katika kuhamahama hawakukaa sana nje ya maeneo ya Kijerumani, tofauti na Wagothi, walileta Italia urithi wa kijenetikia karibu sawa na ule wa watu wa Skandinavia (hasa kisiwa cha Gotland). Mchango huo katika DNA ya Waitalia wa leo kwa jumla hauzidi 10%.

Vilevile katika maeneo walipoishi walichangia mabadiliko ya lugha ya Kilatini kuwa Kiitalia na lugha na lahaja nyingine za Kirumi.

Tanbihihariri chanzo

Vyanzohariri chanzo

Marejeo ya kisasahariri chanzo

Viungo vya njehariri chanzo

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Walombardi kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoShairiJumuiya ya Afrika MasharikiUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaFasihi simuliziNembo ya TanzaniaMshororoMikoa ya TanzaniaVivumishiOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoPentekosteAina za manenoTanzaniaKamusi za KiswahiliMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaOrodha ya makabila ya TanzaniaAfrika Mashariki 1800-1845Orodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaUpendo Furaha PenezaMafurikoMisimu (lugha)KumaKisaweSentensiDiamond PlatnumzKamusi ya Kiswahili sanifuKamusiMisemoMaudhuiSimba S.C.Ukwapi na utaoTanganyikaOrodha ya Watakatifu WakristoNgeliLahaja za KiswahiliMaumivu ya kiunoRoho MtakatifuNomino