Abba Garima

Abba Garima alikuwa mmonaki aliyefanya umisionari katika Ethiopia ya leo akaanzisha monasteri chini ya kanuni ya Pakomi kaskazini kwa Adowa.

Ni kati ya kundi la Watakatifu Tisa wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia wanaosemekana kukimbilia nchi hiyo kutoka sehemu mbalimbali za Dola la Roma[1] kutokana na dhuluma zilizofuata Mtaguso wa Kalsedonia (451). Wengine ni Abba Panteleoni, Abba 'Aléf, Abba Aftse, Abba Guba, Abba Liqanos, Abba Aregawi, Abba Sehma, Abba Yäm'ata (Yemata). Wote walikuwa wamonaki wasomi waliohuisha Ukristo wa Ethiopia. Wanasemekana kuwa ndio watafsiri wa Agano Jipya kwenda lugha ya Ge'ez.[2]

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.