Abrahamu wa Clermont

Abrahamu wa Clermont (Syria, mwishoni mwa karne ya 4 - Auvergne, Ufaransa, 477 hivi) alikuwa mmonaki mwenye asili ya Uajemi. Kutokana na dhuluma ya Wasasani, akiwa bado shemasi, alielekea Misri ili kujifunza ukaapweke lakini mpakani alikamatwa akakaa kifungoni miaka mitano.

Dhuluma iliposimama, alifungulia akaelekea Ulaya magharibi na kuishia Ufaransa alipofanywa padri na abati wa monasteri[1][2][3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Juni [4].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  • Acta Sanctorum June 3:534–536. r. aigrain, Catholicisme 1:57. j. l. baudot and l. chaussin, Vies des saints et des bienhereux selon l'ordre du calendrier avec l'historique des fêtes (Paris 1935–56) 6:251–252.
  • (Kifaransa) Charles-Louis Richard e Jean Joseph Giraud, Bibliothèque sacrée, ou dictionnaire universelle des sciences ecclésiastiques, Parigi, Jacques Rollin, 1760.
  • (Kiitalia) Gaetano Moroni, Dizionario di erudizione storico-ecclesiastica, Venezia, Tipografia Emiliana, 1840, vol. 1º, p. 36 (consultabile anche su Google Libri).
  • (Kiingereza) Frederick George Holweck, A biographical dictionary of saints with a general introduction on hagiology, Saint Louis, Herder Book Co., 1924.
  • (Kireno) Victor Saxer, "Abraão de Clermont", in Dicionário Patrístico e de Antigüidades Cristãs, Petrópolis, Vozes, 2002, p. 31. ISBN 978-85-326-1294-6.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.