Aldegunda

Aldegunda (Cousolre, Ufaransa 639 hivi - Maubeuge, Ufaransa, 684 hivi), alikuwa mwanamke aliyeanzisha monasteri pacha na kuziongoza kama abesi chini ya kanuni ya Kolumbani.

Sanamu ya Mt. Aldegunda huko Hautmont.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu bikira.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Januari[1].

Maisha

Mtoto wa wazazi wa koo mashuhuri, aliongokea Ukristo akabatizwa alifuatwa na baba yake, ambaye akawa baadaye mtakatifu Walbert. Pia mama yake Bertila na dada yake Vatrude[2][3] ni watakatifu[4].

Baada ya kukataa kuolewa, alitawa[5].

Alivumilia kwa ushujaa maumivu ya saratani ya matiti ambayo ikaja kumuua[6].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.