Ali Kiba

Mwanamuziki wa Tanzania
(Elekezwa kutoka Alikiba)

Ali Salehe Kiba (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Ali Kiba; pia: King Kiba; alizaliwa mkoani Iringa, 26 Novemba 1986) ni mwanamuziki wa Tanzania, mwimbaji na mtunzi wa nyimbo chini ya lebo yake ya King's Music records na lebo aliyokuwa akiifanyia kazi Rockstar4000, ambayo alikuwa miongoni mwa wamiliki wake.

Ali Kiba

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwaAli Salehe Kiba
AmezaliwaNovemba 29 1986 (1986-11-29) (umri 37)
Asili yakeIringa, Bendera ya Tanzania Tanzania
Aina ya muzikiMwanamuziki
Kazi yakeMwimbaji Mwanasoka
Aina ya sautiSauti, piano
Miaka ya kazi2006 hadi sasa
StudioRockstars4000
Kings Music
Ame/Wameshirikiana naAslay
Abdu Kiba
Christian Bella
Ommy Dimpoz
M.I
Patoranking
Abby Skills
Mr. Blue

Ana vipaji vilivyo tofauti na wasanii wenzake, hivyo amejikita sehemu nyingine kwa kusajiliwa na timu ya Mpira wa miguu Coastal Union ya mkoani Tanga kucheza mpira wa miguu kwa msimu wa 2018/2019 wa Vodacom Premier League.

Maisha

Ali Kiba alizaliwa na Saleh Omari na Tombwe Njere. Ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wanne kwenye familia yao, akifuatiwa na Abdu Saleh Kiba ambaye pia ni mwanamuziki, Zabib Kiba (dada yake) na Abuu Kiba (mdogo wao wa kiume wa mwisho).[1]

Mafanikio

Mwaka 2011, Ali Kiba alichaguliwa kama msanii wa kwanza wa Afrika Mashariki - Tanzania, Kenya na Uganda.

Kwa mwaka 2015 ameshinda tuzo tano za Kilimanjaro Awards.

Tarehe 20 Mei 2016, kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na muziki "Sony Music Entertainment" ilitangaza kumsainisha mkataba wa kufanya kazi na Ali Kiba.

Tuzo

MwakaKazi iliyoteuliwaTuzoMatokeo
2016HimselfBest International Act: AfricaAmeshinda[2]

Nollywood and African Film Critics Awards

MwakaKazi iliyoteuliwaTuzoMatokeo
2016HimselfFavorite ArtistAmeshinda
MwanaFavorite SongAmeshinda[3]

East Africa TV Awards

MwakaKazi iliyoteuliwaTuzoMatokeo
2016AjeBest Male ArtistAmeshinda
Song of the YearAmeshinda
Video of the YearAmeshinda

ASFA Awards (Uganda)

MwakaKazi iliyoteuliwaTuzoMatokeo
2016AjeMost Stylish Artiste East AfricaAmeshinda
AjeMost Fashionable Music Video AfricaAmeshinda[3]

Soundcity Awards

MwakaKazi iliyoteuliwaTuzoMatokeo
2016AjeVideo of the YearAmeshinda

TZ INSTA Awards 2016

MwakaKazi iliyoteuliwaTuzoMatokeo
2016AjeTop Trending SongAmeshinda

Best Celebrity Player Awards (Uganda)

MwakaKazi iliyoteuliwaTuzoMatokeo
2016HimselfBest Celebrity PlayerAmeshinda

WANNAMusic Awards 2016 (France)

MwakaKazi iliyoteuliwaTuzoMatokeo
2016AjeBest Male ArtistKigezo:Nominated
Best CollaboKigezo:Nominated
People ChoiceAmeshinda

Tanbihi

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ali Kiba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.