Astatini


Astatini (kut. Kigiriki "astateo" (ἀστατέω) "kutodumu" kwa sababu ya unururifu na nusumaisha fupi) ni elementi yenye namba atomia 85 katika mfumo radidia maana yake kiini atomia chake kina protoni 85. Uzani atomia ni 209.98 na alama yake ni At. Ni elementi ya tano katika safu ya halojeni.

Astatini (astatinum)
Jina la ElementiAstatini (astatinum)
AlamaAt
Namba atomia85
Mfululizo safuHalojeni
Uzani atomia 209.98
Valensi2, 8, 18, 32, 18, 7
Ugumu (Mohs){{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka575 K (302 °C)
Kiwango cha kuchemka610 K (337 °C)
Asilimia za ganda la dunia3 · 10-24  %
Hali maada mango
Mengineyonururifu; hutokea wakati wa mbunguo wa Urani

Tabia

Astatini ni elementi ururifu yenye nusumaisha isiyozidi masaa 8.1. Kwa sababu hiyo ni haba sana jumla yake duniani ni takriban gramu 25.

Hujitokeza upya tena na tena katika mbunguo asilia wa urani. Hutengenezwa pia katika maabara.

Kuna matumizi ya kiganga ambako mnururisho wake hutumiwa kuharibu kansa mwilini.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Astatini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.