Brid wa Kildare

(Elekezwa kutoka Brigida wa Kildare)

Brid wa Kildare au Brigid wa Ireland (kwa Kikelti Naomh Bríd; kwa Kilatini Brigida; Faughart, Dundalk, 453 hivi - Kildare, 524 hivi[1][2][3]) ni mmojawapo kati ya watakatifu wasimamizi wa Ireland (pamoja na Patrick na Kolumba).[4]

Kioo cha rangi, Kanisa Katoliki la Mt. Yosefu, Macon, Georgia, 1903.
Mt. Brid, Kikanisa cha Mt. Non, St Davids, Wales.
Msalaba wa Mt. Brid (Crosóg Bhríde).
Brigida wa Kildare, Gross St Martin, Köln, Ujerumani.

Anatajwa kama mmonaki, abesi, na mwanzilishi wa monasteri kadhaa za kike, ikiwemo ile maarufu ya Kildare, ambayo ni kati ya zile za kale zaidi huko Ireland.

Pia mchango wake katika kuendeleza uinjilishaji wa kisiwa hicho uliofanywa na Patrick wa Ireland unaheshimiwa sana hadi leo.

Anahesabiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Februari[5], pamoja na ya Dar Lugdach, mwanafunzi wake aliyerithi mamlaka yake.

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.