Denis wa Korintho

Denis wa Korintho alikuwa askofu wa Korintho (Ugiriki) katika karne ya 2.

Mwenye ujuzi mkubwa wa Neno la Mungu, alielimisha waumini wa mji wake kwa mahubiri na maaskofu wa miji mingine kwa barua.

Mwaka 171 alimuandikia Papa Soter, lakini zimetufikia pia sehemu za barua zake nyingine zinazoonyesha juhudi zake katika utume[1][2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Aprili.

Tazama pia

Tanbihi

Vyanzo

  • Urdang, Laurence. Holidays and Anniversaries of the World. Detroit:Gale Research Company, 1985. ISBN|0-8103-1546-7.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.