Desideri wa Vienne

Askofu wa Vienna

Desideri wa Vienne (kwa Kifaransa: Didier; alifariki 607) alikuwa askofu mkuu wa mji huo na mwanahistoria ambaye aliuawa kwa kupigwa mawe, kwa agizo la malkia Brunhilda wa Austrasia aliyemchukia kwa makaripio yake [1][2][3][4].

Kabla ya hapo alikuwa ameondolewa madarakani kwa kutia shaka uhalali wa watoto wa malkia huyo [5].

Papa Gregori I alimlaumu kwa barua kutokana na juhudi zake za kuelimisha mapadri wake hata kuhusu fasihi[6].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi[7] kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Mei[8].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.