Domnini wa Digne

Domnini wa Digne (alifariki Digne, leo nchini Ufaransa, 5 Novemba 379) alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo kuanzia mwaka 364[1] [2]na wa mji wa Vienne[3].

Mzaliwa wa Afrika Kaskazini, alikwenda Roma mwaka 313 kushiriki sinodi dhidi ya Wadonati akatumwa na Papa Miltiades huko Ufaransa alipoinjilisha sehemu mbalimbali hadi Italia Kaskazini.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[4]

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.