Papa Miltiades

Papa Miltiades alikuwa Papa kuanzia tarehe 2 Julai 311 hadi kifo chake tarehe 10 Januari 314[1]. Kadiri ya Liber Pontificalis, Miltiades alikuwa na asili ya Afrika[2], ingawa aliweza pia kuwa mtu wa Roma.[3]

Papa Miltiades.

Alimfuata Papa Eusebius akafuatwa na Papa Silvester I. Alifurahia amani ambayo Kanisa lilirudishiwa na kaisari Konstantino Mkuu, na ingawa alipingwa sana na Wadonati, alishughulikia kwa busara upatanisho[4].

Wakati wa Upapa wake Hati ya Milano iliwapa wananchi uhuru wa dini (313) na Kanisa lilirudishiwa mali yake iliyotaifishwa.

Alipinga fundisho la Donatus wa Carthago la kwamba mapadri na maaskofu walioasi wabatizwe tena. Uaumuzi huo wa Sinodi ya Laterano (313) haukumaliza uenezi wa farakano la Donato katika Afrika Kaskazini.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[5].

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Miltiades kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.