Emanueli Gonzalez Garcia

Emanueli González García (Sevilia, 25 Februari 1877 – Palencia, 4 Januari 1940) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki, jimbo la Palencia nchini Hispania tangu mwaka 1935 hadi kifo chake.

Mt. Manuel.

Alijulikana kwa ibada kubwa aliyokuwanayo kwa Yesu Ekaristi ambayo alijitahidi kuieneza kotekote. Kwa ajili hiyo alianzisha shirika la Wamisionari wa Ekaristi wa Nazareti, pamoja na yale ya Wanafunzi wa Mt. Yohane na Watoto wa Malipizi.[1]

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 29 Aprili 2001. Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 16 Oktoba 2016.[2][3]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo[4].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.