Emiliani wa Vercelli

Emiliani wa Vercelli (alifariki 11 Septemba 506 hivi) anakumbukwa kama askofu wa 11 wa Vercelli (Italia Kaskazini) kuanzia mwaka 493 au 497 hadi kifo chake[1].

Ingawa alipenda sana maisha ya upwekeni, aliwajibika sana katika uchungaji na maendeleo ya watu wake katika vurugu za uvamizi wa Italia uliofanywa na Waostrogothi, pia kwa kumuunga mkono Papa Simako.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 17 Mei.[2]

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.