Esikyo wa Antiokia

Esikyo wa Antiokia (alifariki Antiokia, leo nchini Uturuki, 303 hivi) alikuwa afisa wa jeshi aliyeuawa kwa kutoswa katika Mto Oronte akiwa amefungwa jiwe kubwa mkononi kwa sababu, wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano dhidi ya Ukristo, alitupa silaha zake aliposikia kwamba asiyekubali kutoa sadaka kwa miungu atapaswa kuacha jeshi [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Mei[2].

Tazama pia

Tanbihi

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.