Filipo Howard

Filipo Howard (28 Juni 155719 Oktoba 1595) alikuwa mtu wa ukoo maarufu nchini Uingereza na binamu wa Malkia Elizabeti I.

Mt. Filipo Howard alivyochorwa.

Baada ya kuishi kwa anasa katika ikulu, alipata uongofu wa kimaadili aliposikiliza hoja za mapadri Wakatoliki (1581) na hatimaye aliacha madhehebu ya Anglikana ajiunge na Kanisa Katoliki, ingawa kwa siri, kutokana na dhuluma ya serikali.

Hatimaye alikamatwa na kufungwa hadi kifo chake miaka 10 baadaye[1].

Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 15 Desemba 1929, halafu Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39[2].

Sikukuu yake ni tarehe ya kifodini chake[3].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.