Isidori mkulima

(Elekezwa kutoka Isidoro Mkulima)

Isidori mkulima (kwa Kihispania San Isidro Labrador, Madrid, Castilia, 1070 hivi – Madrid, 15 Mei 1130[1]) alikuwa mkulima wa Hispania maarufu kwa upendo wake kwa maskini na wanyama.

Mt. Isidori mkulima.
Mt. Isidro na Mt. Maria.

Pamoja na mke wake, mwenye heri Maria wa Cabeza, aliwajibika katika kazi ngumu za shambani, akivuna kwa uvumilivu wake tuzo ya mbinguni kuliko mazao ya ardhi akawa kielelezo cha mkulima Mkristo.

Papa Paulo V alimtangaza mwenye heri tarehe 2 Mei 1619, halafu Papa Gregori XV alimtangaza mtakatifu tarehe 12 Machi 1622.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2] .

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.