Jermano wa Capua

Jermano wa Capua (alifariki Capua, Campania, Italia, 540 hivi) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 516[1].

Mt. Jermano akikutana na shemasi Paskasi ahera (juu kushoto), katika De balneis Puteolanis, kazi ya Petro wa Eboli (karne ya 12).

Kabla ya hapo alikuwa ameuza mali aliyorithi kwa familia yake tajiri ili kusaidia maskini akaishi kitawa.

Rafiki wa Benedikto wa Nursia, tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Oktoba[2].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Marejeo mengine

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.