Katerina wa Aleksandria

Katerina wa Aleksandria (kwa Kigiriki ἡ Ἁγία Αἰκατερίνα ἡ Μεγαλομάρτυς; 282-305 hivi) alikuwa bikira Mkristo wa Aleksandria, Misri ambaye aliuawa kwa amri ya kaisari Maxentius mwanzoni mwa karne ya 4[1].

Mt. Katerina alivyochorwa na Bernardino Luini (National Art Museum of Azerbaijan).
Mchoro wa Artemisia Gentileschi.
Mchoro wa Carlo Crivelli.
Picha takatifu ya Mt. Katerina wa Aleksandria, na vituko vya kifodini chake.

Kadiri ya mapokeo, alikuwa wa ukoo maarufu[2] tena msomi. Kisha kuongokea Ukristo akiwa na umri wa miaka 14, aliongoza watu mia kadhaa kumfuata katika dini hiyo[3].

Tangu alipofia dini anaheshimiwa na Wakristo wa madhehebu mbalimbali kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Novemba au 25 Novemba.[4][5][6]

Picha

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

  • Allen, Prudence, The concept of woman: the Aristotelian revolution, 750 BC-AD 1250, 1997 (2nd edn.), Wm. B. Eerdmans Publishing, ISBN 978-0-8028-4270-1
  • Walsh, Christine. The Cult of St Katherine of Alexandria in Early Medieval Europe, (Ashgate 2007)

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.